Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza  timu ya Simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika baada ya kuibamiza vibaya timu ya US Gendarmerie 4-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpambano huo ambapo amesema  ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.

"Ninaipongeza Timu ya Simba kwa ushindi  wa kishindo kuelekea kwenye Robo Fainali ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika. Kama Taifa, tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza Nchi yetu kimataifa." Amefafanua Mhe. Mchengerwa


Ameitaka Timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha   ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea kuitangaza Tanzania duniani.

Simba kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).

Ukiachilia timu hizi nne(4) timu nyingine  nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids (Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.

Simba inatarajiwa  kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa.

Comments

Popular posts from this blog

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Maafisa Utamaduni na Michezo tekelezeni maagizo ya Waziri Mkuu kwa Vitendo - Mhe Mchengerwa

FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA