Posts

Showing posts from February, 2022

Mhe. Mchengerwa apongeza watanzania kuongoza Kili Marathon 2022

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon na kuongoza katika mbio hizo tofauti na miaka ya nyuma ambapo mataifa mengine yamekuwa yakiongoza. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Februari 28, 2022 na kufafanua kuwa mwitikio huo mkubwa umetokana na kazi nzuri ambayo iliyofanywa na Rais wa  Samia Suluhu Hassan toka akiwa Makamu wa Rais ambapo aliongoza kuhamasisha riadha na kuanzishwa kwa klabu za mazoezi (jogging clubs) kwenye kila mkoa hapa nchini. Aidha amesema mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali ya sasa kwenye Sekta ya michezo inakwenda kuleta mapinduzi makubwa ikiwa ni pamoja na kutoa ajira nyingi kwa wananchi. Katika mashindano hayo mtanzania Alyce Simbu aliongoza  kilomita 42  aliyetumia muda wa 02:16:30 wakati kwenye kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu zilichukuliwa na watanzania zikiongozwa na Emmanuel Ginniki (01:00:34), akifua...

MHE. GEKUL AELEZA MIKAKATI YA KUKUZA RIADHA KILI MARATHONI

Image
  Na. John Mapepele  Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathoni huku akifafanua kwamba tukio hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo nchini  inayosisitiza ushiriki wa pamoja kati ya Serikali na wadau  katika kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo riadha.  Mhe. Gekul ameyasema hayo leo Februari 27, 2022 wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ili atoe hotuba yake kwenye kilele cha mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, 2022 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.  “Sisi familia ya michezo tunajivunia uwepo wa tukio kubwa namna hii linalowaleta pamoja wanamichezo na wapenzi wa riadha kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yetu, kipekee niwapongeze Kilimanjaro Premium Lager kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza michezo hapa nchini”. Amesema Mhe. Gek...

MHE. MCHENGERWA ATEMBELEA MAONESHO YA DUBAI EXPO

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa   ametembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO Dubai 2020 yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu na kupongeza  waoneshaji baada ya kujionea jinsi Tanzania inavyotumia   maonesho hayo ya Kitamaifa kujitangaza.  Mhe, Mchengerwa. jana Februari 24, 2022 amepita kukagua kwenye mabanda hayo ya maonesho na kuhimiza utoaji wa maelezo kiufasaha ili wageni wanaotembelea mabanda hayo  watambue vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini hatimaye wafike kutembelea Tanzania. Katika mabanda hayo, Tanzania inajitangaza  kupitia fursa mbalimbali za Utalii, Madini, Nishati, Kilimo na Uwekezaji kwa wageni.  Mbali na maonesho ya kuonesha fursa mbalimbali pia Tanzania kwa mara ya kwanza imeutambulisha Utamaduni wa Tanzania kupitia muziki wa singeli duniani katika maonesho haya kupitia  mfalme wa singeli nchini Sholo Mwamba ambaye amewache...

MHE. MCHENGERWA ATAKA SINGELI IITEKE DUNIA DUBAI EXPO LEO

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii wanaopanda leo Februari 24,2022 kuiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho makubwa ya kimataifa ya Dubai Expo, Mfalme wa Singeli Sholo Mwamba na Mkongwe wa Muziki wa Asili wa Tanzania Mrisho Mpoto kuendelea kutoa burudani ya kukata na shoka ili kuitangaza Tanzania kimataifa.  Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Februari 24,2022 wakati ambapo Sholo Mwamba anatarajia kuendelea kuwaipagawisha dunia kwa nyimbi za singeli  majira ya saa 11:00 jioni  kwenye ukumbi wa *Earth Stage* baada ya  kufanya  vizuri kwenye onesho lake  la awali Februari 22, 2022 na kuwaacha  umati uiliofika   kucheza naye huku wengine wakichukua picha kwa ajili ya matumizi yao. “Tunataka Singeli na muziki wa kwetu uiteke dunia ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza  vizuri safari ya mapinduzi makubwa  ya sanaa kwenye anga za kimataifa” amesisitiza Mhe. Mchenge...

MAMA NA MICHEZO

Image
 

Mhe. Mchengerwa awaalika wananchi Tamasha la Serengeti

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwenye tamasha kubwa Tanzania na Afrika la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival) litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma ili kujionea hazina ya vipaji vya wasanii nchini. Mhe. Mchengerwa amesema haya, hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa tamasha hili ndiyo tamasha kubwa linaloratibiwa na Serikali likiwa na lengo la kuibua vipaji vya wasanii pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuliingizia taifa mapato kutokana na hazina ya utalii uliopo.  Aidha, amesema tamasha hilo litahusisha wasanii zaidi ya hamsini wa miziki ya aina mbalimbali ambao watatumbuiza   ili kuleta vionjo na radha tofauti tofauti.  “Tamasha hili linaleta muunganiko wa kipekee kabisa linaloonyesha tasnia ya burudani na utalii na ndiyo maana tumetumia jina la Mbuga yetu bora Afrika na duniani ya Serengeti ili kuwavutia wageni kutoka sehemu m...

MAELEKEZO YA MHE. MCHENGERWA YAFIKIA PAZURI

Image
  Na. John Mapepele  Maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ya kutaka mchakato wa mwaka huu wa utoaji wa Tuzo za Muziki  bila upendeleo  yamefika  mahali pazuri. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko, leo Februari 21, 2022 imeeleza kuwa jumla ya kazi 402 zimewasilishwa kuanzia Februari 9, 2022 baada ya zoezi la kuwaelimisha wadau kukamilika na kuwa BASATA limeamua kuongeza muda wa siku saba ili kutoa nafasi kwa wasanii wengi kushiriki. “Tunaongeza siku 7 kwa ajili ya wasanii kuwasilisha kazi katika vipengele vya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2021)” imefafanua taarifa hiyo.  Pia taarifa hiyo imefafanua kwamba mwisho wa kuwasilisha kazi hizo ni Machi mosi mwaka huu kupitia link www. tanzaniamusicawards.info  Akizungumza kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Utoaji wa Tuzo za Muziki na Ugawaji wa Mirahaba kwa Wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nye...