Posts

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusai...

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA)  kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge      kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa  yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili  rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya   wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili  zisainiwe  na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii  wafaidi matunda ya...

FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Image
Na John Mapepele Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino  amesema  FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo. Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania. Akiongozana na wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi  Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania. "Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine" amefafanua Mhe. Mchengerwa Aidha, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo. Mh...

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha  Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea  jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua  mashindano maalum ya soka y...

MHE. MCHENGERWA - CAF KUZINDUA “AFRIKA SUPER CUP

Image
  Na John Mapepele- Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Omary Mchengerwa amesema Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) unaofanyika kesho Agosti 10,2022 jijini Arusha Tanzania, unakwenda kuzindua mashindano maalum ya kandanda ya Afrika Super CUP. Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Arusha leo, Agosti 9, 2022 Mhe. Mchengerwa amesema mkutano huo ambao ni wa kwanza wa kihistoria katika Bara la Afrika na Tanzania unafaida kubwa kiuchumi na kimichezo.  Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa baadhi ya wageni wanaoshiriki kwenye mkutano huo wameshapanga kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii hapa nchini baada ya kumalizika kwa mkutano huo. Mchengerwa amesema mkutano huo wa 44 unatarajiwa kufanyika kesho ambapo unajumuisha mataifa 58 na nchi 54 ni za Afrika. Aidha, amesema ni nchi mbili tu za Afrika yaani Kenya na Zimbabwe ambazo zinatumikia adhabu ambazo hazishiriki kwenye mkutano huo. Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa CAF Dkt....

Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili

Image
  Na John Mapepele,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana  na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili  katika  mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia  ombi lake alilolitoa  kwa  shirika  la UNESCO wakati wa siku ya  maadhimisho ya Kiswahili duniani   mwaka huu iliyofanyika  kwa mara ya  kwanza  Julai 7, 2022.  Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya  Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka  ya   Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume  hiyo siku  tano  kukamilisha andiko  hilo ili liwasi...

Rais Samia awamwagia madola wachezaji Jumuiya ya Madola- Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  amesema  Serikali inakwenda kutoa zawadi kwa wachezaji wote watakaoleta medali za mashindano ya madola yanayoanza nchini Uingereza hivi karibuni kama hamasa maalum kwa wachezaji. Amesema kwa mara ya kwanza  kabisa Serikali imeandaa zawadi dola  10000 kwa mshindi atakayerejea na medali ya dhahabu na  dola 7000 kwa mshindi wa medali ya fedha  na mshindi atakayeshinda  medali ya shaba atapata dola za kimarekani 5000. Mhe, Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 20, 2022 kwenye hafla ya  kuwaaga wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam amewataka wachezaji kuweka uzalendo mbele na kuwataka kurudi na medali. Amefafanua kuwa watambue kwamba dhamira ya Serikali kwa sasa ni kufanya mapinduzi makubwa ambapo amesisitiza kuwa watanzania wamechoka w...