Posts

Showing posts from April, 2022

Mhe Gekul awataka watanzania kutumia fursa za Royal Tour

Image
  Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb) amewataka watanzania  kutumia  fursa iliyotengenezwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan   kwenye Filamu ya Royal Tour. Mhe. Gekul ameyasema  haya leo Aprili 29, 2022 kwenye  semina ya wadau wa sekta ya filamu ya Royal Tour katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. Naibu  Waziri Gekul amesisitiza kuwa Serikali Serikali ipo tayari kushirikiana na wanatasnia ya filamu katika kuendeleza Sekta ya filamu nchini ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi yatakayo wawezesha wanatasnia wa ndani na nje ya nchi kufanya shughuli zao nchini. Aidha, amesema yapo maeneo  kadhaa muhimu ambayo Tanzania inaweza kushirikiana na Marekani katika filamu na ikanufaika nayo. Ameyataja maeneo hayo  kuwa ni pamoja  na utayarishaji wa filamu kwa kutumia mandhari zinazo pat...

Waziri Mchengerwa atoa siku tatu kwa Bodi ya Filamu Tanzania kutekeleza maelekezo yake

Image
  Na. John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa leo Aprili 23, 2022 amefanya ziara ya kikazi kwenye taasisi ya Bodi ya Filamu nchini (TFB) na kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha na kuleta mapinduzi kwenye tasnia Filamu nchini ambapo ametoa siku tatu za kufanyia kazi maelekezo kadhaa aliyoyatoa.  Mhe. Mchengerwa amesema tasnia ya filamu inazalisha ajira na kutoa mchango mkubwa kwenye taifa hivyoTFB inatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kasi ili kuleta mapinduzi yanayositahili kwenye sekta hiyo hapa nchini. Akiwakilisha baadhi ya mikakati ya TFB, kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo,     Mtendaji Mkuu wa Taasisis hiyo, Dkt. Kilonzo Kiagho amesema taasisi hiyo imejiwekea mikakati kabambe ambayo inaendana na miongozo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.  Ameitaja baadhi ya mikakati itakayoleta mageuzi makubwa kwenye tasnia hiyo kuwa ni pamoja na kuanzisha tozo la filam...

Kinana aipongeza Wizara kwa kuhifadhi Utamaduni wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Image
  Na John Mapepele Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara. Mhe, Abdulrahman Kinana leo Aprili 20, 2022 ametembelea Ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jijini Dar es Salaam na kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya kupata maelezo ya Waziri anayeisimamia Wizara hiyo, Mhe. Mohamed Mchengerwa. Mhe. Kinana amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo uti wa mgongo wa taifa lolote na kusifu jitihada zinazofanywa na Wizara kwenye kuhakikisha  utamaduni wa kiukombozi wa Bara la Afrika  unaenziwa na kuhifadhiwa kwa faida ya sasa na  vizazi vijavyo. Kwa upande wake, Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa mpango wa Serikali kwa sasa  ni kujenga makumbusho kubwa ya kisasa. Aidha, amesema  programu  inaendelea  na kushirikiana  na Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha mchakato wa kuyatangaza maeneo15 ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika yaliyopo nchini kuwa...

Wadau wekezeni kwenye miundombinu ya michezo - Mhe, Mchengerwa

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amemwakilisha, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim  Majaliwa Majaliwa kwenye ufunguzi wa maabara ya kisasa ya Komputa iliyojengwa kwa ufadhili wa klabu ya Baseball Dodgers ya Marekani kupitia Chama cha Mchezo wa Baseball/Softball Tanzania. Tukio hilo amelifanya leo, Aprili 19, 2022 kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa taasisi za michezo wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  Saidi Yakubu na wadau mbalimbali. Mhe. Mchengerwa ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuwekeza katika miundombinu ili sekta ya michezo iweze kusonga mbele Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali  ni kuendelea kukuza sekta ya Michezo na Sanaa kwa kushikiana na wadau wenye utashi wa kuwekeza katika sekta hizo. "Mpango wa Serikali ni kufanya michezo iwe biashara".ameongeza  Mhe, Mchengerwa Aidha, amesema tayari Serikali imeweka mazingir...

Hongereni Simba- Mhe, Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya  Simba kwa ushindi wa  goli 1-0 dhidi timu ya Orlando Pirates Aprili 17, 2022 kwenye dimba la  Mkapa  jijini Dar es Salaam. Pongezi hizi ameendelea kuzitoa leo baada ya zile alizotoa jana mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo. Ikumbukwe kuwa Mhe. Mchengerwa jana aliwaongoza maelfu ya  watanzania kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan kuishangilia Simba katika uwanja wa Mkapa hatimaye ikatwaa ubingwa huo. Asubuhi kabla ya mechi hiyo, Mhe. Mchengerwa baada ya kumaliza kushiriki mashindano makubwa  ya Qur'an barani Afrika  yaliyofanyika kwenye uwanja huo huo wa Mkapa, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu  wake Said Yakubu alitoa wito kwa watanzania kujitokeza kuja kuishangilia Simba katika mechi hiyo iliyochezwa kuanzia  saa moja usiku ili ishinde. Ubingwa wa Simba ulipatikana kupitia kwa beki kisiki Sho...

Mhe Mchengerwa atoa wito kwa wananchi kushiriki sensa, anuani za makazi

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mazoezi ya kitaifa ya uandikishaji wa anuani ya makazi na sensa yanayoendelea hivi sasa nchini kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Mhe, Mchengerwa ameyasema haya leo wakati akiongea na wananchi wa vijiji vya Mgomba, Ngorongo na Kilimani kwenye Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Amefafanua kwamba  mazoezi haya yana faida kubwa kwa nchi yetu  kwa kuwa yanasaidia kupanga  mipango mbalimbali ya maendeleo kwa muda wa sasa  na baadaye. Aidha, ameishukuru Serikali   ya awamu ya sita kwa kukamilisha mipango ya maendeleo katika kipindi kifupi. Ametaja baadhi ya mipango ambayo inatekelezwa kuwa ni pamoja na  miundombinu ya barabara, shule na vituo vya afya na jengo la kujifungulia akina mama ambapo amewataka wananchi kutumia na kusimamia vizuri raslimali zinazotolewa. Aidha ameipongeza...

Maafisa Michezo simamieni vikundi vya mazoezi- Mchengerwa

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewaagiza maafisa michezo nchi nzima kuvisajili vikundi vyote vya mbio za hisani (Marathon) katika wilaya zao na kuvifuatilia ili kutoa motisha kwa vikundi vinavyofanya vizuri na  kuwaandaa wanariadha  kushiriki mashindano ya kimataifa na kusaidia kuzuia maradhi mbalimbali. Mhe, Mchengerwa ametoa agizo hilo leo, Aprili 10, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za hisani kwa ajili ya utoaji wa elimu na ufahamu kuhusu usonji zilizo andaliwa na taasisi ya Usonji ya Lukiza. Ameongeza kuwa wanariadha hao bora watakaopatikana kupitia mbio mbalimbali watashiriki mashindano ya kimataifa na kuliletea taifa medali mbalimbali. Akizungumzia mashindano ya Jumuiya ya madola, Waziri Mchengerwa amesema washiriki wote watakao kwenda kushiriki katika michezo hiyo Serikali inawahudumia, na wote wapo kambini wakiendelea kujiandaa vyema kuwakabili washindani wao katika m...

Mhe.Mchengerwa- Serikali Kuboresha Sekta ya Filamu

Image
    Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo imekuja na nguvu kubwa ili kuleta maboresho na mabadiliko ya kisasa katika ukuaji wa Sekta ya Filamu nchini.  Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Aprili 9, 2022 alipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Mhe. Waziri ambaye aliongozana na viongozi kutoka Kampuni ya Nichani ya India ikiongozwa na Bw. Manu Nichani na Trans Innova ya Marekani ikiongozwa na Dkt. David Faria, amesema lengo la kuja kwa viongozi hao ni kuona namna gani wanaweza kutusaidia kufanya mabadiliko ya pamoja na kupata uzoefu katika sekta ya filamu.  “Dhamira ya Serikali ni kuleta mapinduzi ya dhati katika Sekta ya Filamu na tumedhamiria kweli kweli kuitoa hapa ilipo na kuipeleka mbele zaidi,” alisema Mhe. Mchengerwa. Mhe. Waziri amesema Wizara kupitia mashirikiano baina ya Kampuni hizo mbili itafanya mambo makubwa ambayo watanzania watayafurahia na yatadumu kwa kizazi cha leo na cha baadae. Mhe. Waziri amesema, wataalam ha...

Mhe Mchengerwa , Trans Innova na M- Nichan Group wakubaliana kuwekeza Kwenye Sanaa na Michezo

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa leo Aprili 7, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Kampuni ya Trans Innova na  M-Nichani Group zote kutoka nchini India na kukubaliana kuwekeza katika sekta za Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam ambapo wawekezaji hao wameonesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta za utamaduni, sanaa na michezo. Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mchengerwa amewashukuru  wawekezaji hao kwa kuwa tayari kuunga mkono sekta hizo ambazo ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwani zinatoa ajira kwa vijana wengi. "Tunaahidi kushirikiana na nyinyi ili kukuza sekta hizi na kupitia Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tutaweza kufanikisha hili kwani tuna mpango wa kukijenga ili kiwe kituo cha mafunzo ya sanaa na filamu Tanzania", alisema Mhe. Mchengerwa. Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa M-Nichani Group Bwana Manohar Nicha...

Maafisa Utamaduni na Michezo tekelezeni maagizo ya Waziri Mkuu kwa Vitendo - Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo  kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa Waziri Mkuu jana Aprili 5, 2022 wakati akifungua  kikao kazi cha maafisa hao na  kuwataka  kutumia utaalaam  wao kufanya kazi kwa weledi Katika kuendelea kuwapa  furaha  watanzania. Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Aprili 6, 2022 wakati alipokuwa akimkaribisha Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao hicho cha siku tatu kilichojadili mambo mbalimbali ya sekta hizo. “Naomba nendeni mkawe karibu na wananchi pia muwe wanyeyekevu kwa sababu tukiwa karibu na wananchi mambo  mengi yatakwenda  vizuri” amesisitiza Mhe. Mchengerwa. Akizungumzia  kuhusu uwajibikaji amesema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alihusia   kila mtu akitekeleza wajibu wake maendeleo ya haraka yanawezekana ambapo ametoa wito,  kwa maafisa hao kwenda tufanya mageuzi ...