Posts

Showing posts from August, 2022

FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Image
Na John Mapepele Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino  amesema  FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo. Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania. Akiongozana na wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi  Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania. "Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine" amefafanua Mhe. Mchengerwa Aidha, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo. Mh...

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha  Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea  jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua  mashindano maalum ya soka y...

MHE. MCHENGERWA - CAF KUZINDUA “AFRIKA SUPER CUP

Image
  Na John Mapepele- Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Omary Mchengerwa amesema Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) unaofanyika kesho Agosti 10,2022 jijini Arusha Tanzania, unakwenda kuzindua mashindano maalum ya kandanda ya Afrika Super CUP. Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Arusha leo, Agosti 9, 2022 Mhe. Mchengerwa amesema mkutano huo ambao ni wa kwanza wa kihistoria katika Bara la Afrika na Tanzania unafaida kubwa kiuchumi na kimichezo.  Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa baadhi ya wageni wanaoshiriki kwenye mkutano huo wameshapanga kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii hapa nchini baada ya kumalizika kwa mkutano huo. Mchengerwa amesema mkutano huo wa 44 unatarajiwa kufanyika kesho ambapo unajumuisha mataifa 58 na nchi 54 ni za Afrika. Aidha, amesema ni nchi mbili tu za Afrika yaani Kenya na Zimbabwe ambazo zinatumikia adhabu ambazo hazishiriki kwenye mkutano huo. Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa CAF Dkt....

Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili

Image
  Na John Mapepele,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana  na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili  katika  mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia  ombi lake alilolitoa  kwa  shirika  la UNESCO wakati wa siku ya  maadhimisho ya Kiswahili duniani   mwaka huu iliyofanyika  kwa mara ya  kwanza  Julai 7, 2022.  Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya  Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka  ya   Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume  hiyo siku  tano  kukamilisha andiko  hilo ili liwasi...